Mshezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Taifa na Club ya VIJANA- ‘CITY BULLS’ Alphaeus David Kisusi anatarajiwa kuondoka nchini jumanne ya tarehe 17/1/2012 kuelekea nchini Canada Kimasomo kufuatia Scholraship aliyoipata Katika Chuo Kikuu cha NEWFOUND MEMORIAL.
Mwaka jana mwezi wa nane MAMBO BASKETBALL pamoja na Tanzania Students Achievement Organisation (TANSAO) ambayo ni asasi sisizo za kiserikali walifanya mafunzo ya mpira wa kikapu (Basketball Camp) iliyoongozwa na Coach Peter Benoite toka katika chuo kikuu cha Newfound Memorial kwa nia ya kutoa nafasi (Partial schorlaship) kwa mchezaji wa ki-Tazania ambapo Alphaeus alifanikiwa baada ya kukidhi mahitaji ya kupata nafasi hiyo ambayo yalikuwa ni uwezo wa kucheza Mpira wa kikapu na matokeo mazuri kimasomo. Alphaeus pamoja na kucheza katika timu ya chuo hicho atakuwa akisomo kozi ya ‘International Business’ kwa miaka 3.

Alphaeus alizaliwa mwaka 1992, Ana urefu wa futi sita na inchi 3, Kilo 74 na anacheza nafasi ya ‘shooting guard’. Ni mtoto wa tatu katika familia ya Bwana David na Elizabeth Kisusi. Amemaliza elimu ya sekondari kidato cha sita katika shule ya kimataifa ya Academic iliyopo jijini Dar es salaam. Alianza kucheza mpira wa kikapu baada ya kuhamasishwa na kaka yake aitwaye Joseph ambae ni mchezaji katika timu ya CHUI ya hapa DSM na akajikuta akiacha kujihusisha na michezo mingine aliyocheza akiwa na umri wa miaka 12.
Pamoja na kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya mchezo huu Alpha katika kipindi cha miaka 4 iliyopita alifanikiwa kwenda Senegal na kuhudhuria katika mafunzo yaliyo chini ya NBA yajulikanayo kama ‘Basketball Without Border’ BWB. Alikuwa ni miongoni mwa wachezaji 3 wa kitanzania walichaguliwa kwenda Marekani mwaka Jana kufuatia mafunzo ya wacheazi wa zamani toka Marekani yaliyofanyika hapa Dar es salaam. Msimu ulipoita alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika ligi daraja la kwanza ambapo aliiongoza timu yake ya VIIJANA kushika nafasi ya tatu.
NI matumaini ya MAMBO BASKETBALL kuwa Alphaeus atakuwa mfano wa kuigwa na wachezaji wanoibukia, pia itakuwa changamoto kubwa kwa wachezaji walioko mashuleni haswa wale jijini Mwanza ambapo kwa kushirikiana tena na Program ya mpira wa kikapu ya Newfound Memorial university tunatarajia kufanya mafunzo mengine mwezi wa saba mwaka huu jijini mwanza na Arusha. Nafasi hiyo ya masomo itatolewa tu kama atapatikana mchezaji atakayekidhi vigezo vikuuu ambavyo ni uwezo kielimu na kimchezo.
MAMBO BASKETBALL inamtakia kila la heri na kuwapongeza sana wazazi wa Alphaeus ambao katika kipindi chote wamekuwa wakihakikisha kuwa ana-balance kati ya shule na michezo, pia kutoa wito kwa wachezaji vijana walioko mashuleni kukazania masomo kwani ndio ufunguo wa kila jambo na ili ufanikiwe kimichezo SHULE NI LAZIMA! Pongezi nyingine ziende kwa wadau wote wa mpira wa kikapu TBF, BD, Wachezaji na vyombo vya habari ambao kwa njia moja au nyingine wamefanikisha ndoto hii kutimia.
No comments:
Post a Comment