Jan 10, 2012

BAA YAUZA BIA KWA MBWA WANAOFUATANA NA WATEJA

Mbwa aitwaye Franco akifaidi bia maalum kwenye baa ya Branding Villa. 

MTEJA anayefika kwenye baa ya Branding Villa huko Gosforth, Newcastle, Uingereza, akiwa na mbwa wake, sasa anaweza kuagiza bia maalum kwa ajili ya mnyama huyo.Bia hiyo ambayo huwa haina mapovu, hutengenezwa kwa kimea na vitu vya kuongeza ladha.

Meneja wa baa hiyo, Dave Carr, amesema bia hiyo ilianza kuuzwa ili kuleta mazingira bora kwa ajili ya mbwa wanaofuatana na wateja wao.Hatua hii imechukuliwa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wanyama hao zaidi mbali na utaratibu uliopo sasa wa kuwapa bakuli na maji na biskuti maalum za mbwa.

Meneja huyo ameliambia gazeti la Daily Mail kwamba mbwa wote wameipenda bia hiyo, na kwamba iwapo wanyama hao hawataridhika kikamilifu na kinywaji hicho, bado wanaweza kuridhika na vyakula vya kwenye baa hiyo ambayo ni maalum kwa wanyama hao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...