Jan 9, 2012

DIAMOND, WENZAKE WAHUKUMIWA JELA MIEZI 6, WALIPA FAINI

Diamond (kulia) na mcheza shoo wake wakiwa nje ya mahakama ya mwanzo mjini Iringa leo asubuhi muda mfupi kabla ya kuhukumiwa.

MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ na wenzake wamekubali kosa la kumshambulia mwandishi Francis Godwin na kuhukumiwa kwenda jela miezi sita kila mmoja ama kulipa faini ya shilingi elfu hamsini (50,000/=) kwa kila mmoja ikiwa ni pamoja na kulipa shilingi elfu thelathini (30,000/=) kwa Godwin.

Watuhumiwa wamelipa faini hiyo japo mwanahabari huyo hajapokea fedha hiyo na anakusudia kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...