Jan 7, 2012

Diamond kupanda kortini jumatatu


NYOTA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumatatu atapanda kwenye kizimba cha Mahakama ya Wilaya, Iringa akikabiliwa na msala wa kuharibu mali.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, msanii huyo anatakiwa kutinga mahakamani hapo asubuhi ya saa 2:30, bila kukosa huku ikisemekana mlalamikaji alilazimika kufungua kesi hiyo kufuatia mlalamikiwa kupuuza makubaliano.

Diamond ambaye yumo ndani ya mgogoro mkubwa na aliyekuwa mchumba’ake, Wema Sepetu, alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Iringa siku moja kabla ya kuingia kwa mwaka mpya wa 2012 akidaiwa kuharibu mali ya mwandishi wa habari, Francis Godwin.

Katika sakata hilo, Diamond alitakiwa kumlipa mwandishi huyo Sh. milioni 1.8, lakini akaomba hadi Sh. milioni 1.7 na kumuomba msahama yaishe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...